JIFUNZE KUTENGENEZA JUISI YA TIKITI MAJI NA LIMAO

JUISI YA TIKITI MAJI NA LIMAO NOI SAFI SANA SANA


MAHITAJI

5 kg ya Watermelon
180gram juice ya limao
80 gram ya asali mbichi
1 fungu majani ya Mint
vipande vya barafu au Ice Cubes,

JINSI YA KUTENGENEZA FATILIA PICHA NA MAELEZO HAPO CHINI

Muda wa maandalizi : dakika 15

Muda wa mapishi : dakika 15
Idadi ya wanywaji : Watu 4



Kiwango cha limao kinaweza kua gram 120 hadi gram 240 hii hutegemea na kiwango cha sukari katika tikiti maji au



Kata kata watermelon katika vipande vidogo, menya ngozi na kumbuka kutoa mbegu.





Chukua vipande vya watermelon saga pamoja na juice ya limao





Kisha ichuje katika chujio safi baada ya kuisaga





Kisha weka ice cube pamoja na majani ya mint katika jagi.





Kisha mimina juice katika jagi lako lenye barafu na mint





Kisha mimina asali mbichi kwenye mchanganyiko wa juisi na ukoroge ichanganyike.





Kihsa mpatie mnywaji ikiwa ya baridi weka ice cubes na majani ya mint kwa kupambia.





Huu ni muonekano safi kabisa baada ya kupamba kwa jani la mint na kuongeza ice cubes ili mnywaji afurahie kinywaji baridi






KINYWAJI HIKI NI SAFI SANA NA KINONGEZA HAMU YA KULA WAAANDALIE FAMILIA WABURUDIKE

Comments

Popular posts from this blog

JIFUNZE KUTENGENEZA JUISI YA KAROTI NANASI NA TANGAWIZI

JIFUNZE KUTENGENEZA JUISI YA EMBE BICHI